Man U, Marseille nguvu sawa

Olympic Marseille ya Ufaransa imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kutoka sare tasa na Manchester United ya England.

Image caption Marseille watoka sare na United

United ambao walisafiri kwenda Ufaransa bila ya wachezaji wao watano wa kikosi cha kwanza walihimili vishindo vya Marseille.

Hata hivyo haukuwa mchezo wa kusisimua sana kama michezo mingi katika ngazi ya 16 bora ya klabu bingwa Ulaya.

Haki miliki ya picha g
Image caption Mario Gomez

Katika mchezo mwingine, mabingwa watetezi Inter Milan ya Italia nayo imeshindwa kutamba mbele ya Bayern Munich ya Ujerumani baada ya kufungwa 1-0.

Goli ya Bayern Munich limefungwa na Mario Gomes katika dakika ya 90.