Idhaa za BBC zakamilisha kazi

Ijumaa tarehe 25 Februari 2011, ni siku ambayo itakuwa ya mwisho kwa matangazo ya lugha tano za idhaa za BBC.

Image caption Idhaa tano za BBC zafunga kazi

BBC imekuwa ikirusha matangazo kwa lugha ya Ki Serbia tangu mwaka 1939 idhaa ya Yugoslavia ilipoanzishwa. Idhaa hiyo iliendelea hadi mwaka 1991 ilipotenganishwa kati ya Serbia na Coatia kufuatia vita vya huko Balkan.

Itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Agosti mwaka 1944, idhaa ya Yugoslavia, baada ya kuanzishwa miaka mitano kabla ilibeba jukumu kubwa la kuwapasha habari takriban watu milioni 20 waliokumbwa na balaa la nchi yao kutekwa na utawala wa Kinazi.

Kazi kubwa ya kuwapasha raia hao habari zisizoegemea upande wowote likawa jukumu la wandishi wa idhaa hiyo, ingawa waliothubutu kuisikiliza walikabiliwa na hatari ya kukamatwa au hata kuuawa.

Idhaa hiyo iliendelea kwa miaka mingine hamsini hadi mwaka 1991, juhudi za Uhuru wa kujitenga ulipozuka huko Slovenia, Croatia na Bosnia.

Hivyo idhaa ya Yugoslania ikagawanywa mara mbili: Serbia na Croatia, ingawa idhaa ya Croatia ilifungwa mnamo mwaka 2005.

Kupitia kipindi kigumu cha muongo wa 1990, wakati serikali ya Slobodan Milosevic ikijitahidi kuziba sauti za vyombo huru, idhaa ya Serbia iliendelea kupeperusha matangazo.

Wasikilizaji wake waliongezeka wakati wa dhiki na matatizo, mfano wakati NATO iliposhambulia Serbia wakati wa vita vya Kosovo.

Hilo huenda lingewafanya raia wa Serb waichukie serikali ya Uingereza kwa kuongoza mashambulio hayo lakini wasikilizaji wa idhaa ya Serb waliendelea kuisikiliza.

Zaidi ya miaka kumi tangu Milosevic apinduliwe, Taifa imara la Serbia yenye utawala unaofuata demokrasia limejitokeza likijitahidi kuwmwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Hoja ni kwamba umuhimu wa kuhitaji idhaa ya lugha ya Ki-Serb umepungua kutokana na kwamba nchi hiyo imejenga vyombo vyake vya utangazaji na habari pamoja na taasisi za kutegemewa.

Hivyo basi, baada ya huduma ya miaka 72 tangu BBC ianze kupeperuha matangazo yake kwa lugha ya Wa-Serb wenyewe, matangazo hayo yamesikika kwa mara ya mwisho leo ijumaa tarehe 25 mwezi wa pili mwaka 2011 na nchi nzima inaiaga BBC na idhaa ya Kiserb iliyowahudumia kupitia vipindi vigumu katika historia ya eneo hilo.

Kwa upande mwingine majirani wa wa Swahili barani Afrika, na ofisini, Wareno wanaopeperusha matangazo yao Afrika, wakiwa na wasikilizaji milioni moja na nusu nchini Msumbiji peke yake, walianza matangazo yao mnamo mwaka 1930 na kukata matangazo hayo alfajiri ya ijumaa tareh 25 mwezi febuari mwaka 2011.

Licha ya kufunga matangazo ya Rediyo, idhaa hiyo ijukanayo kama BBC Mundo itaendelea kujenga mawasiliano yake kupitia tovuti.

Idhaa ya BBC ya matangazo ya dunia inasema imechukuwa uwamuzi mgumu wa kufunga idhaa hizo kutokana na uwamuzi wa kupunguza matumizi kama ilivyotakiwa na serikali.