Ferguson aiondoa Chelsea katika ubingwa

Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameiondoa Chelsea katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu ya soka ya England, kabla hawajapambana siku ya Jumanne katika uwanja wa Stamford Bridge.

Haki miliki ya picha

Chelsea kwa sasa wapo nyuma ya Manchester United wanaoongoza ligi kwa pointi 12, huku Arsenal wanaoshikilia nafasi ya pili wakionekana ni wapinzani wakuu kwa sasa katika kinyang'anyiro hicho.

Meneja wa Shetani Wekundu Ferguson, pia amepuuza maneno ya nahodha wa Chelsea, John Terry kwamba United nayo itajikwaa.

"Kwa kawaida timu hizo mbili zinakuwa zimeshafahamu muelekeo wao inapofika mwishoni mwa msimu- na hivyo ndivyo inavyoonekana," aliongeza Ferguson.

"Nadhani kama sio sisi basi watakuwa Arsenal kushinda ubingwa msimu huu."

United, ambao mwaka 2009 walitawazwa mabingwa wa England kwa mara ya 18, wataongeza wigo wa pointi nne zaidi na kuendelea kujishindilia kileleni mwa ligi dhdi ya Arsenal, iwapo watashinda mchezo wao dhidi ya Wigan siku ya Jumamosi.

Ushindi huo pia utawaweka Shetani Wekundu pointi 15 mbele ya Chelsea, ambao mwishoni mwa wiki hii hawacheza.