Stoke yatoka sare na WBA 1-1

Vela
Image caption Carlos Vela

Carlos Vela wa West Brom nusura aipatie klabu yake pointi zote tatu baada ya kukosa nafasi za wazi katika dakika za majeruhi.

Stoke City waliongoza kwa bao la kichwa la Rory Delap katika dakika ya 57.

Dakika tatu kabla ya kumalizika kwa mchezo Carlos Vela alisawazisha goli hilo ambalo lilionekana kama la kuotea.

Pointi hiyo moja imeiondoa West Brom katika mkia wa ligi hadi katika nafasi ya 17, na kukaa juu ya Wolves, West Ham na Wigan inayoburuza mkia.

Stoke wakicheza nyumbani wanasalia katika nafasi 10 wakiwa na pointi 34.