Carling Cup: Mc Leish apongeza mafanikio

Meneja wa Birmingham Alex McLeish, amesema ushindi wa timu yake wa Kombe la Carling dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Wembley, umekuwa ni "mafanikio makubwa" akiwa meneja.

Obafemi Martins alifunga bao la ushindi dakika ya mwisho ya muda wa kawaida na kuiwezesha timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya the Gunners.

"Nimefurahishwa sana na mashabiki, wamekuwa wakiusubiri ushindi kwa muda mrefu," McLeish ameiambia BBC.

"Kusema ukweli, ni mafanikio yangu makubwa. Kwa klabu ndogo kama yetu kuifunga Arsenal ni mafanikio makubwa kupindukia."

Birmingham had taken the lead through Nikola Zigic but Robin van Persie equalised for the Gunners at a packed Wembley.

McLeish alishawahi kuiongoza klabu ya Rangers kuchukua ubingwa wa ligi mara mbili na vikombe mara tano alipokuwa meneja wa timu hiyo na ushindi unaokumbukwa wa Scotland dhdi ya Ufaransa mwaka 2007.

Alieleza zaidi: "Nilipokuwa na Rangers nilikuwa nikitumaini kushinda vikombe, ingawa ilikuwa vigumu dhidi ya Celtic. Kuja England na klabu kama ya Birmingham kuifunga klabu kubwa ya Arsenal, kwangu mimi ndoto yangu imetimia.