Chelsea yainyuka United

Chelsea imeichapa Manchester United mabao 2-1 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Image caption Frank Lampard

United ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Chelsea kwa mkwaju mkali ulioachiwa na Wayne Rooney katika dakika ya 29.

David Luiz wa Chelsea alisawazisha bao hilo katika dakika ya 54 kwa shuti kali.

Dakika kumi kabla ya kumalizika kwa mchezo Frank Lampard alifunga bao la ushindi la Chelsea kwa mkwaju wa penati, baada ya beki wa United Chris Smalling kufanya makosa ndani ya eneo la hatari.

Nemanja Vidic alipewa kadi yekundu baada ya kumuangusha Ramirez nje kidogo ya eneo la hatari.

Ushindi wa Chelsea umeipeleka hadi katika nafasi na nne ikiwa na pointi 48.

Manchester United imesalia na pointi 60, nne zaidi ya Arsenal iliyopo nafasi ya pili, ikiwa na mchezo mmoja zaidi.