FA ya Misri yapunguzia mishahara

Chama cha soka nchini Misri (EFA) kimetangaza kitapunguza mishahara ya wafanyakazi wake.

Image caption Wachezaji wa timu ya taifa ya Misri

Wachezaji wa timu ya taifa nao huenda mishahara yao ikipunguzwa.

Taarifa iliyotolewa kupitia mtandao wa EFA imeeleza hakuna mfanyakazi yeyote ndani ya chama hicho atakayepokea mshahara unaozidi dola 2,500, wakati mshahara wa kima cha chini utakuwa ni kiasi cha dola 250.

Hivi karibuni Misri ilikumbwa na tafrani za kisiasa, hali iliyosababisha kusimamishwa shughuli za soka nchini humo kiasi mapato yamepungua.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza uamuzi huo "unakwenda sambamba na hisia za mapinduzi".

EFA pia wamesema watakutana na vilabu vya soka nchini humo kukubaliana taratibu za fidia kwa wachezaji watakaoitwa katika timu ya taifa.