Mbunge aliyevaa herini afukuzwa bungeni Kenya

Mbunge mmoja nchini Kenya amefukuzwa nje ya bunge kwa kuvaa mavazi yasiyo na heshima.

Mbunge huyo wa jimbo moja mjini Nairobi,Gidion Mbuvi,alifukuzwa kwenye kikao cha jana kwa kuvaa miwani ya jua na herini ndogo za mawe yenye thamani.

Naibu spika wa bunge, Farah Maalim, alisema namna bwana Mbuvi alivovaa haionyeshi heshima kwa bunge,ambalo halijawahi kuwa na mbunge mwanamume aliyevaa hereni. Naibu spika wa bunge alishtumiwa na wafuasi wa Mbuvi kwa kukosa uvumilivu.

Mbuvi anajulikana kama Sonko -- jina ambalo kwa lugha ya mtaani linamaanisha mtu tajiri anayeishi maisha ya kifahari.