Mtuhumiwa wa shambulio Mali atoroka

Mtuhumiwa aliyeshambulia ubalozi wa Ufaransa nchini Mali ametoroka jela.

Image caption Bamako, Mali

Afisa kutoka ofisi ya rais nchini Mali amekataa kutoa maelezo zaidi jinsi mtuhumiwa huyo, raia wa Tunisia, alivyotoroka.

Watu wasipoungua wawili walijeruhiwa katika tukio hilo ambapo mabomu yalirushwa katika ubalozi huo uliopo Bamako.

wakati mabomu yalilipuliwa gerezani humo iliyoko Bamako.

Polisi walisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa mwanachama wa Al-Qaeda kitengo cha Afrika Kasakazini lakini kundi hilo halijatoa kauli yoyote kuhusu shambulio hilo.

Shirika la habari la AFP imeripoti kuwa mkuu wa idara ya ujasusi ya Mali amesimishwa kazi kwa sababu ya tukio hilo.

Kitengo cha Al-Qaeda kinachoendeleza shughuli zake katika nchi za kiislamu Afrika kaskazini, kimetekeleza mashambulio kadhaa nchini Mali na nchi za jirani.

Hali hii imeibuka kutokana na makundi ya wapiganaji wa kiislamu waliokuwa wanapigana Algeria miaka ya 90.