Waziri Mkuu wa Misri amejiuzulu

Waziri Mkuu wa Misri Ahmed Shafiq amejiuzulu

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Ahmed Shafiq

Baraza la jeshi lilitoa taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo aliyekuwa waziri wa usafiri, Essasm Sharaf, amependekezwa kuunda serikali mpya.

Bw Shafiq aliteuliwa kuwa waziri mkuu siku chache tu kabla ya Rais Hosni Mubarak kujiuzulu tarehe 11 Februari baada ya siku kadhaa za maandamano

Waandamanaji walisema kuwa Bw Shafiq alikuwa mshirika wa karibu sana wa Bw Mubarak.

Baraza kuu la jeshi lilikubali uamuzi wa Bw Shafiq na kumteua Essam Sharaf kuunda serikali mpya lilisema jeshi hilo kupitia ukurasa wao wa face book.

Jumatatu, Misri ilimwekea vikwazo ya kutosafiri Hosni mubarak na familia yake.