Wakanusha kudhibiti miji Libya

Miji minne ya nchini Libya ambayo majeshi yanayomtii Kanali Muammar Gaddafi yalidai kuidhibiti imesalia mikononi mwa wapinzani, kwa mujibu wa watu waliopo katika maeneo hayo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mapigano imeendelea Libya

Tobruk na Ras Lanuf, imesalia mikononi mwa waandamanaji, walisema waandishi wa habari wa BBC.

Majeshi yanayompinga Kanali Gaddafi, yanashikilia miji ya Misrata na Zawiya, kwa mujibu wa habari za wapinzani na wakazi wa huko.

Lakini Misrata na Ras Lanuf ilishambuliwa siku ya Jumapili, na pia mapigano yameripotiwa katika mji mdogo wa Bin Jawad.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wapinzani

Mjini Tripoli, maafisa walisema milio ya bunduki iliyosikika saa za alfajiri ilikuwa ya wapinzani wakisherekea kudhibiti miji.

Watu wengi awali walidhani milio hiyo ilikuwa ni mapigano kati ya majeshi ya wanaomtii na wanaompiga Kanali Gaddafi, na pia kuna tetesi kuwa hiyo milio ya buduki ya kusherekea ilikuwa kisingizio cha kufunika mapigano.

Tripoli imekuwa ngome kuu ya Kanali Gaddafi, wakati akijitahidi kurejesha udhibiti wa nchi kutoka kwa wanaompinga, ambao wamechukua eneo kubwa la upande wa mashariki, na pia katika miji ya karibu na Tripoli, upande wa magharibi.