Carlo Ancelotti aondoa tamaa ya ubingwa

Meneja wa Chelsea, Carlo Ancelotti ametupilia mbali nafasi ya timu yake kutetea ubingwa wa Ligi Kuu, licha ya kuilaza Blackpool 3-1.

Image caption Carlo Ancelotti

Ushindi huo umeifanya Chelsea ipitwe kwa pinti tisa na vinara wa ligi hiyo Manchester United, wakiwa na mchezo mmoja kibindoni watakaocheza na Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.

Lakini Ancelotti amesema: "Lengo letu kwa wakati huu ni kubakia katika timu nne bora.

"Tunazidi kuwasogelea Manchester United, lakini hatuna budi kujiandaa kwa mchezo ujao na kujiandaa vizuri kwa kila mechi."

"Kwa sasa tupo nyuma kwa pointi tisa na tuna mchezo dhidi ya Birmingham, lakini ni jambo ambalo si rahisi kufikiria kama tutaweza kutetea ubingwa wetu."

Chelsea sasa wamekusanya pointi 51 wakishikilia nafasi ya nne.