Japan kinu cha nuklia chatatiza

Waziri Mkuu wa Japani, Naoto Kan, amesema nchi yake inakabili janga kubwa kabisa, tangu vita vya pili vya dunia, wakati nchi inajaribu kushughulikia maangamizi yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi na tsunami.

Wakati wakuu wanajaribu kuzuwia kinu cha umeme cha nuklia huko Fukushima, kisipasuke kabisa, imesema kuwa kinu chengine, kiko katika hali ya hatari.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wajapani wanapimwa viwango vya miyale ya nuklia

Shirika la Atomiki la Kimataifa, IAEA, limesema karibu na eneo lilopigwa vibaya na Tsunami, la Onagawa, kiwango cha miyale ya nuklia kiliongezeka. Wahandisi wamejaribu, kupooza tanuri katika kinu kimoja, kwa kutumia maji ya chumvi.

Huku nyuma kazi za uokozi zinaendelea, na katika eneo moja lilopigwa na tsunami, inahofiwa watu kama elfu kumi wamekufa.