Nigeria yahitaji tume maalumu uchaguzi

Serikali ya Nigeria imehimizwa kuanzisha tume maalumu itayochunguza na kuchukua hatua za kisheria, dhidi ya ghasia na upotovu wowote utaotokea wakati wa uchaguzi.

Image caption Ramani ya Nigeria

Wito huo umetolewa na shirika la kimataifa la kupigania haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, na shirika la mawakili wa Nigeria.

Katika taarifa ya pamoja, mashirika hayo yamesema kwamba Nigeria inahitaji kuhakikisha kuwa fujo, vitisho na udanganyifu hautochafua uchaguzi mkuu wa mwezi ujao.

Mashirika hayo yamesema ingawa watu 50 wameuwawa katika fujo za uchaguzi tangu mwezi Novemba, hata hivyo polisi hawana uwezo na uhuru wa kuchunguza mauaji hayo na hakuna mtu aliyekamatwa.