West Ham nje

Klabu ya Stoke imejiunga na Manchester United pamoja na Bolton kushiriki hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Meneja wa West Ham, Avram Grant

Hiyo ni baada ya kuifunga West ham kutoka mashariki mwa jiji la London 2 - 1.

Hivyo Westham ikawa klabu ya mwisho kutoka jiji la London kuondolewa katika michuano ya FA baada ya Arsenal kufungishwa virago na Manchester United siku ya jumamosi ilipoifunga 2 - 0.

Ikumbukwe kuwa Westham ilishindwa kufunga bao la mkwaju wa peneti dakika ya 47 kabla ya Danny Higginbotham kufunga bao la ushindi kupitia mkwaju wa free-kick uliompita mikononi goalkeeper wa West Ham.

Bolton ilifuzu kushiriki nusu fainali baada ya kuitwanga Birmingham city bao 3-2.

Bao la ushindi la Bolton likipatikana katika dakika ya 90 kupitia Mkorea Lee Chung-Yong.

Ratiba 16 Aprili

Tayari ratiba ya nusu fainali imeisha pangwa na mshindi wa mchuano baina ya Manchester city na Reading atapambana na Manchester united katika nusu fainali tarehe 16 Aprili.

Bolton ichuane na Stoke.