Wafuasi wa Gbagbo washambuliwa

Wafuasi wa Alassane Outtara wamewashambulia wafuasi wa rais Laurent Gbagbo katika mji mkuu wa Abidjan nchini Ivory Coast.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mfuasi wa Ouattara

Milio ya risasi ilisikika Jumatatu tarehe 14 jioni katika wilaya mbili zilizoko karibu na kambi la jeshi.

Mwandishi wetu wa BBC, John James, aliripoti kuwa tukio hilo litachochea mzozo unaoendelea nchini humo bila kuipelekea nchi hiyo kuingia katika hali ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Rais Gbagbo amekataa kuachia madaraka ilhali Bw Ouattara anatambuliwa na wengi kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa urais mwaka jana.

Hii ni mara ya kwanza ya kuzuka mapigano katika kitongoji cha Yopougon ambacho kinamuunga mkono Bw Gbagbo, na kile cha Adjame cha wafuasi wa Bw Ouattara.

Mwandishi wetu alisema hakuna uhakika kama wafuasi wa Ouattara wamepiga hatua au wamekuwa tu wakitekeza mashambulio katika maeneo ambayo wana uashawishi mkubwa.