Mapambano Brega, Libya

Mapigano kati ya jeshi la Libya na waasi yameshika kasi huko mjini Brega.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waasi mjini Brega, Libya

Wakati mmoja pande zote mbili zilidai kuwa zimedhibiti mji huo.

Magharibi mwa nchi hiyo jeshi la libya lilisogea karibu na mji wa Zuwara na pia kulishambulia mji wa Misrata.

Jumuiya ya nchi nane tajiri duniani G8 imetoa wito kuchukuliwa hatua dhidi ya Kanali Muammar Gaddafi lakini hawakutaja marufuku ya ndege kutopaa katika anga ya Libya.

Afisa mmoja kutoka Umoja wa Mataifa ametoa wa kukomesha mashambulio dhidi ya waandamanaji na kuzingatia kuwepo na uwezo wa kutoa huduma za kibinaadamu.

Ndege za serikali zimekuwa zikiyashambulia kwa mabomu maeneo ya mipakani ya mji wa Ajdabiya.

Kulingana na taarifa kutoka AFP, milio ya miripuko ilisikika ikiongezeka mjini humo na huduma za dharura za kuwaondo majeruhi mjini humo na kuwapeleka hospitalini zimeongezeka.

.