Maharamia wahukumiwa Marekani

Maharamia wahukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama ya marekani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mharamia wa kisomali

Wasomali watano wamehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuishambulia manuwari ya jeshi la wanamaji la Marekani waliodhani ni manuwari ya bidhaa.

Wanaume hawo watano walipatikana na hatia mwezi Novemba kwa kujaribu kuiteka nyara manuwari ya USS Nicholas iliyokuwa katika operesheni ya kudhibiti tatizo la maharamia.

Mawakili wa upande wa utetezi wamedai kuwa watu hao walikuwa mateka na walilazimishwa kufyatua risasi wakati waliposhambuliwa mwezi Aprili.

Waendesha mashtaka walisema hii ni mara ya kwanza watu kuhukumiwa katika kesi ya maharamia na jopo la mahakama la marekani tangu mwaka 1820.