Jeshi lashambulia mji wa Ajdabiya, Libya

Waasi wamekanusha madai kuwa wafuasi wa Gaddafi wameudhiti mji wa Ajdabiya.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ghasia Libya

Mwandishi wetu Jon Leyne akiwa mjini Benghazi alisema kuwa jeshi liliushambuliwa mji huo ardhini kwa mara ya kwanza.

Wakati jeshi linaposogea karibu na mji huo na kutekeleza mashambulio, baraza la usalama la umoja wa mataifa linazungumuzia swala la ndege kutopita katika anga ya Libya.

Viongozi wa waasi wanataka jumuiya ya kimataifa kumzuia Gaddafi na jeshi lake kutumia ndege kuwashambulia.