Lehmann arejea Arsenal

Jens Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jens Lehmann

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa golikipa Jens Lehmann anafanya mazoezi na klabu hiyo na atatia saini mkataba hadi mwisho wa msimu.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 41, amekuwa mchezaji huru tangu alipostaafu soka mwaka 2010, baada ya kuichezea Stuttgart.

Makipa wengine wa Arsenal Wojciech Szcezesny, Lucasz Fabianski na Vito Mannone ni majeruhi, huku Manuel Almunia akiwa kipa pekee aliyesalia.

Lehmann aliichezea Arsenal mara 199 kati ya mwaka 2003 hadi 2008.

Kwa kuwa hana klabu yoyote anayochezea, Arsenal haitalazimika kulipa ada ya kumsajili, na anaweza hata kuichezea Arsenal siku ya Jumamosi dhidi ya West Brom.

Wenger alisema: "Lehmann anafanya mazoezi nasi, na atasaini mkataba hadi mwisho wa msimu".