Ferguson apongeza mwenendo wa wachezaji

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amefurahishwa na "mwenendo" wa wachezaji wake kufuatia ushindi wao wa bao 1-0 dhdi ya Bolton Wanderers.

Image caption Sir Alex Ferguson

Bao la Dimitar Berbatov dakika ya 88, huku Arsenal wakitoka sare ya 2-2 dhidi ya West Brom, limeipeleka United kileleni zaidi kwa tofauti ya pointi tano.

"Huo ndio mwenendo wa klabu hii," alisema Ferguson.

"Vilabu vingine vinakosa hili nchini England. Sisi ni wazuri sana kupata kitu dakika za majeruhi."

Ushindi katika uwanja wa Old Trafford umekuja baada ya Manchester United kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Chelsea na Liverpool, na kufanikiwa kusonga mbele katika Kombe la FA na Ubingwa wa Ulaya kwa kuzifunga Arsenal na Marseilles.

"Tulikuwa na mechi tano ngumu kwa wiki kadha zilizopita, aliongeza Ferguson, aliyekuwa akiangalia pambano hilo akiwa jukwaani uwanja wa Old Trafford akianza kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi tano kukaa kwenye benchi la ufundi.