Makaazi ya Kanali Gaddafi yashambuliwa

Ndege zake za kijeshi, zimeshambulia makaazi ya Kanali Gaddafi mjini Tripoli na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye jengo moja.

Viongozi wa muugano wa majeshi hayo wanasema jengo lililoharibiwa lilikuwa linatumika kuamrisha majeshi ya Libya yanayopigana na waasi.

Waandishi wa habari wametembezwa kwenye eneo hilo lakini hakuna taarifa ikiwa maafa yalitokea baada ya shambulizi hilo.

Naibu mkuu wa jeshi la wanamaji wa marekani Bill Gortney anasema mashubulizi hayo hayaja mlenga kanali Gaddafi.

Haki miliki ya picha Reuters

Televisheni ya Libya imeonesha maiti na magari ya kijeshi yaliyoteketea kwenye barabara ya kuelekea mji wa Benghazi, shina la wapinzani wa serikali

Msemaji wa serikali ameeleza kuwa watu 64 wameuwawa katika mashambulio yaliyofanywa na mataifa ya magharibi, lakini hakuna njia ya kuthibitisha taarifa hiyo.

Awali afisa mkuu wa jeshi la Marekani, , Mike Mullen, alisema ndege kutoka Qatar zinapelekwa huko, kuwa tayari kushiriki katika operesheni dhidi ya Libya, na nchi nyengine piya zimetoa ahadi kusaidia.

Adimeri Mullen alieleza kuwa agizo la Umoja wa Mataifa, la kuzuwia ndege za serikali kuruka katika anga ya Libya, sasa limetekelezwa, na majeshi ya Kanali Gaddafi, katika mji wa Benghazi, unaodhibitiwa na wapinzani, sasa hayawezi kusonga mbele.

Alisema hakuona taarifa, kuwa raia wameuwawa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption mpinzani na bunduki yake karibu na Benghazi

Urusi imetoa wito kwa Uingereza, Ufaransa na Marekani, ziache kushambulia maeneo yasiyokuwa ya kijeshi, na kwamba raia wameshambuliwa.

Mkuu wa Jumuiya ya Kiarabu, Amr Moussa, amesema mashambulio yamekwenda mbali, kushinda lile lengo la kulinda tu anga ya Libya, ambavyo ndivo jumuiya yake ilivotaka.