Hatumlengi Gaddafi - Majeshi

Majeshi ya ushirika yanayoendesha mashambulio ya anga yanasema Kanali Muammar Gaddafi sio lengo lao, licha ya kushambulia makazi yake usiku.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ndege ya kivita

Mkuu wa jeshi la Marekani kikosi cha Afrika Jenerali Carter F Ham amesema kumshambulia Gaddafi sio sehemu ya mpango wao.

Msemaji wa jeshi la Ufaransa, amesema hata kama watafahamu kiongozi huyo wa LIbya yuko wapi, hawatamshambulia.

Umoja wa Mataifa ulipitisha muswada wa kulinda raia, wakati Kanali Gaddafi akipambana na waasi, katika ghasia zilizozuka mwezi uliopita.

Siku ya Jumapili, waziri wa ulinzi wa Uingereza Liam Fox alisema kumlenga Gaddafi huenda "ukawa uwezekano".

Hata hivyo siku ya Jumatatu, mkuu wa majeshi wa Uingereza Jenerali Sir David Richards alisema kumlenga Kanali Gaddafi pekee "hairuhusiwi chini ya muswada wa Umoja wa Mataifa".