Terry akiri kuwepo kwa mgawanyiko

John Terry amekiri kuwa ni kweli atakuwa na upinzani baada ya kurejeshwa tena kuwa nahodha wa timu ya England.

Image caption John Terry

Terry alivuliwa unahodha, kufuatia taarifa tuhuma katika maisha yake binafsi miezi kumi na tatu iliyopita.

Hata hivye amerejeshwa, na Rio Ferdinand kuvuliwa nafasi hiyo.

"Najua sitapendwa na wote" amesema John Terry ambaye pia ni naodhwa wa Chelsea, ambaye anadai kwa sasa ana busara zaidi.

Imeelezwa Ferdinand ameshitushwa na jinsi kocha wa England Fabio Capello alivyolishughulikia suala hili.