Waasi wateka miji zaidi Libya

Waasi wa Libya wamechukua udhibiti wa miji mingine minne na wanasogea haraka kuelekea katika ngome ya Muammar Gaddafi katika mji wa Sirte.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waasi wakiwa Ras Lanuf

Waasi hao wamechukua miji ya mashariki ya Ras Lanuf, Brega, Uqalya na Bin Jawad, baada ya majeshi yanayomuunga mkono Gaddafi kuodoka kufuatia shinikizo la mashambulizi ya anga kutoka kwa majeshi ya ushirika.

Waasi hao pia walidhibiti bandari ya Ajabya siku ya Jumamosi.

Ndege za Marekani, Ufaransa, Uingereza na mataisfa mengine washirika, walianza kushambulia majeshi ya serikali ya Libya siku nane zilizopita.

Nguvu za kijeshi zilifikiwa baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha hatua za kulinda raia.

Wajumbe wa Nati wanakutana mjini Brussels siku ya Jumapili, huku wakitarajiwa kujadili jinsi ya kupambana nchini LIbya na pia kuongeza shughuli zake za kijeshi.