Hasara ya maandamano ya Syria

Serikali ya Syria inasema watu 12 waliuwawa katika maandamano ya Jumamosi, wakati fujo zilipozuka katika maandamano ya kupinga serikali katika mji wa pwani wa Latakia.

Watu kama 200 piya walijeruhiwa, pale watu wasiojulikana na waliokuwa na silaha, waliosimama mapaani, walipofyatua risasi dhidi ya raia.

Wakuu wanasema, waliouwawa wengi ni raia na askari wa usalama.

Rais Bashar al-Assad wa Syria anatarajiwa kuhutubia taifa, baada ya maandamano dhidi ya serikali ya zaidi ya juma moja.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii