Barry nahodha England dhidi ya Ghana

Meneja wa England Fabio Capello, amemteua Gareth Barry kuwa nahodha kwa ajili ya mechi ya kirafiki siku ya Jumanne, dhidi ya Ghana katika uwanja wa Wembley.

Barry, mwenye umri wam miaka 30, atakiongoza kikosi cha England kutoka kile kilichoilaza Wales 2-0 kwenye michuano ya kufuzu kwa Kombe la Euro 2012 siku ya Jumamosi, huku Andy Carroll ataanza katika safu ya ushambuliaji.

Capello alimrejeshea unahodha wa England John wiki iliyopita na kueleza kwa nini alizungumza na Steven Gerrard lakini si nahodha aliyepokonywa hatamu Rio Ferdinand.

"Rio alikuwa nahodha, kwa hiyo ni lazima nikutane naye. Steve ni makamu nahodha," aliongeza Capello.

Capello, ambaye amekiri mwishoni mwa wiki kufanya makosa juu ya suala zima la unahodha, baada ya kumrejesha Terry ambaye pia ni nahodha wa Chelsea, akaongeza: "Natumaini nitazungumza na Rio wiki ijayo."

"Nawaheshimu mashabiki. Itapendeza kwao kuwaona wachezaji wasiowafahamu vyema." Siku ya Jumapili, Gerrard - ambaye amejeruhiwa na hayumo katika kikosi cha England kwa sasa, alibainisha Capello alimpigia simu kumuelezea uamuzi wake wa kumrejeshea Terry unahodha, wakati Ferdinand - ambaye naye ni majeruhi - hajawasiliana na meneja.

Capello amesema atabadilisha "wachezaji kiasi saba" kwa ajili ya mechi dhidi ya Ghana, ambao katika mashindano ya Kombe la Dunia yaliyopita walifika hatua ya robo fainali na kubainisha sababu zake za kuwaruhusu Terry, Frank Lampard, Ashley Cole, Wayne Rooney na Michael Dawson kurejea katika vilabu vyao.

"Baadhi ya wachezaji wamecheza mechi nyingi," alisema Capello. "Wanatakuiwa kucheza mechi tatu tu katika kipindi cha siku nane - Nadhani mechi nne katika muda wa siku 10 inachosa sana. Naheshimu vilabu nawachezaji.