Maandamano dhidi ya serikali yaanza Syria

Rais wa Syria Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais wa Syria

Ripoti kutoka nchini Syria zinasema kuwa maandamano ya kupinga serikali ya nchi hiyo yameanza katika miji kadhaa nchini humo.

Walioshuhudia maandamano hayo katika mji wa kusini wa Deraa, wameiambia BBC kuwa, mamia ya watu waliotoka sala za ijumaa walijumuika na waandamanaji wengine kwenye maanndamano hayo.

Hali ya ulinzi imeimarishwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Damascus.

Wanaharakati wa kisiasa wameahidi kile wanachokiita siku kuu ya wafa dini ili kuwakumbuka watu waliouawa kwenye maandamano ya kisiasa nchini humo katika muda wa wiki mbili zilizopita.

Siku ya Jumatano Rais wa nchi hiyo , Bashar al-Assad alishindwa kutuliza waandaamanaji hao wakati alipohutubia taifa hilo, huku akiyalaumu mataifa ya kigeni kwa kuchochea maandamano dhidi ya serikali yake.