Kashfa ya Simu India

Wakuu wa India wamemshtaki waziri wa zamani wa mawasiliano ya simu pamoja na makampuni matatu makubwa ya simu za mkononi, kutokana na tuhuma kwamba walihusika katika ile inayoweza kuwa kashfa kubwa kabisa ya ulaji rushwa nchini humo.

Kashfa hiyo imelinyima taifa dola bilioni 60.

Waziri huyo, Andimuthu Raja, ameshtakiwa kwa kufanya njama, udanganyifu na kula rushwa.

Mashtaka hayo yanahusu kandarasi ya mwaka 2008, ya kuuza leseni za simu za mkononi, kwa bei ndogo sana, kulingana na thamani halisi.

Bwana Raja amekanusha tuhuma hizo.

Alilazimika kujiuzulu mwaka jana.

Kashfa hiyo imechafua sifa ya serikali ya muungano.