India yashinda Kombe la Dunia Kriketi

India imeichapa Sri Lanka na kunyakua Kombe la Dunia la mchezo wa Kriketi.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mashabiki wa India

India taifa linalopenda sana mchezo huo imechukua ubingwa huu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1983.

Sri Lanka ilipiga 91 katika overs 10 za mwisho, na kupata mikimbio 274-6, huku Mahela Jaywardene akipata mikimbio 103.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Nahodha Mahenda Singh Dhoni

India ilimpoteza Virender Sehwag na Sachin Tendulkar mapema, lakini Gautam Gambhir na Mahendra Dhoni waliimarisha mitupo.

Gambhir alitolewa akiwa na 97, lakini nahodha Dhoni akiwa na 91, bila kutolewa, aliifikisha India kwenye ushindi huku wakiwa wamesaliwa na mipira 10 ya kurusha.