Japan Kinu cha Nuklia Kina Ufa

Kampuni inayomiliki kinu cha nishati cha nuklia kilichoharibika, huko Fukushima, Japan, inasema maji yenye mionzi ya nuklia, yanamwagika baharini kutoka ufa ulioko kwenye shimo la saruji la kinu nambari mbili.

Haki miliki ya picha Reuters

Wakuu wa kampuni ya Tepco, wanasema, ufa huo, huenda ukawa ndio chanzo cha kuvuja huko, na wanajitayarisha kuziba ufa kwa saruji.

Majuma matatu baada ya kinu hicho kuharibiwa na tetemeko la ardhi na tsunami, Waziri Mkuu, Naoto Kan, amezuru kituo kinachotumiwa na mafundi wanaojaribu kurekibisha uharibifu, katika eneo la kilomita 20, linalozunguka kinu.