NATO yapiga wapiganaji wa Libya kimakosa

Serikali ya Libya, imekataa pendekezo la kusitisha mapigano, lilotolewa na upinzani. Msemaji wa serikali ya Libya alisema, huo ni mtego tu.

Image caption Wapiganaji wa Libya

Jana usiku ndege za NATO zililenga mji wenye mafuta, wa Brega.

Na taarifa moja inasema, ndege moja ya NATO, jana usiku ilipiga msafara wa wapiganaji karibu na mji wa Ajdabiya, wakati msafara huo uanaelekea Brega, na inaarifiwa watu 15 waliuwawa.

Hakuna aliyeshangaa kuwa serikali ya Libya, imekataa haraka, pendekezo la upinzani, la kusitisha mapigano, na kwamba majeshi ya serikali, yaache ku-izingira miji ya magharibi, na iruhusu uhuru kamili wa kujieleza. Msemaji wa serikali, alielezea pendekezo hilo kuwa mtego.

Kwa hivo pande zote mbili, hazina hamu kwa sasa, ya kutafuta amani. Serikali imei-komboa ardhi kubwa iliyokuwa imetekwa na wapiganaji hivi karibuni, kwa sababu serikali ina jeshi lenye silaha na mafunzo bora.

Wapiganaji wana-jiamini, kwa sababu NATO iko upande wao, na wanachotaka ni Kanali Gaddafi aondoke. Wapiganaji wamekuwa wakiwatuma wanajeshi wenye mafunzo mstari wa mbele, na kujaribu kuwaweka nyuma, wapiganaji wa kujitolea, ambao hawana mpango.

Kwa hivo baada ya kusonga mbele na kurudi, kama ilivotokea katika majuma mawili yaliyopita...kwa sasa, mapigano yamekwama, na yanatokea katika mji wenye mafuta, wa Brega, kama maili mia-moja magharibi ya ngome ya wapinzani, yaani mji wa Benghazi.