Maandamano Mengine Afghanistan

Watu kama watano wameuwawa kusini mwa Afghanistan, wakati wa maandamano mengine ya kupinga kuchomwa kwa Kuran, huko Marekani.

Zaidi ya watu 40 wengine walijeruhiwa wakati wa mapambano na polisi mjini Kandahar.

Haki miliki ya picha AP

Walioshuhudia tukio hilo, wanasema waandamanaji walichoma moto mipira ya magari na walishambulia maduka na ofisi.

Hapo jana, shambulio dhidi ya kituo cha Umoja wa Mataifa huko Mazar-i-Sharif, wakati wa maandamano mengine dhidi ya kuchomwa moto Kuran, yaliuwa watu 14, wakiwemo wafanyakzi wa Umoja wa Mataifa.

Baadhi ya wakuu wameilaumu Taliban kwa mashambulio hayo, lakini Taliban wamekanusha kuhusika.

Maandamano yanafuatia video inayoonesha Kuran ikichomwa mbele ya kasisi mmoja wa Marekani.