City yatoa onyo kali

Manchester City imesogea hadi nafasiya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya England baada ya kuitandika Sunderland mabao 5-0.

Image caption Yaya Toure

City wamewaata kauli wakosoaji kwa kuonesha mchezo maridadi, tofauti na jinsi walivyokuwa wakicheza katika siku za hivi karibuni.

Adam Johnson aliandika bao la kwanza baada ya kupasiana vyema na Yaya Toure.

Carlos Tevez aliandika bao la pili kwa mkwaju wa penati, katika dakika ya 15.

David Silva alipachika bao la tatu, huku la nne likifungwa na Patrick Vieira na Yaya Toure kufunga la tano katika dakika ya 73.

City wameingia katika nafasi ya tatu licha ya kuwa wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Chelsea.

Mapema, Fulham ilishinda mchezo wake dhidi ya Blackpool.

Mabao mawili ya Bobby Zamora na moja la Dickson Etuhu yaliizamisha Blackpool na kuipeleka katika nafasi ya 11.