Uchaguzi wa Nigeria Umeahirishwa Tena

Uchaguzi wa Nigeria umeahirishwa tena.

Tume ya Uchaguzi (INEC) ilisema uchaguzi wa wabunge sasa utafanywa Jumamosi, tarehe 9 Aprili, na uchaguzi wa rais na magavana utacheleweshwa hadi baadaye mwezi huu.

Uchaguzi uliotarajiwa kufanywa Jumamosi, awali uliahirishwa hadi Jumatatu, lakini sasa imetangazwa tarehe mpya.

Sababu ya kuahirishwa ni matatizo ya uratibu.

Jumamosi kulizuka ghadhabu, baada ya mkuu wa Tume ya Uchaguzi, Professor Attahiru, kukiri kuwa zana za kupigia kura hazikuwasili katika vituo.

Waandishi wa habari wanasema, kuahirishwa huko ni pigo kubwa kwa Nigeria, ambayo ikijaribu kusahau historia ya upigaji kura wenye dosari.