Majeshi ya UN yamshambulia Gbagbo

Helikopta za Umoja wa Mataifa na za Ufaransa zimeshambulia kambi za kijeshi zinazoongozwa na kiongozi aneyekataa kuondoka madarakani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, katika hatua ya kuzua raia kushambuliwa.

Mashambulio hayo yamekuja wakati wapiganaji wanaomuunga mkono hasimu wa Bw Gbagbo, Allasane Ouattara wakiongeza jitihada zao za kuchukua udhibiti wa mji wa Abidjan.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukishinikizwa kutekeleza azimio lake la kulinda raia, na kuomba msaada wa Ufaransa.

Makundi ya kimataifa yanasema Bw Ouattara ndio kiongozi halali wa nchi hiyo.

Waangalizi na mashirika ya eneo hilo yanasema alishinda uchaguzi mwaka jana, lakini Bw Gbagbo amegoma kuondoka madarakani.

Katika siku za hivi karibuni, majeshi yanayomuunga mkono Bw Ouattara yameanzisha mashambulio makali, kuanzia upande wa kaskazini na kuchukua karibu nchi yote.

Watu walioshudia hatua hiyo walisema hakukuwa na upinzani mkali wakati majehi ya Ouattara yakitekeleza hatua hiyo hadi kufika Abidjan, ambayo ndio ngome ya Bw Gbagbo.