Mkasa wa ajali ya Ndege watokea Congo

ramani ya Congo
Image caption Visa vya ajali ya ndege vinatokea mara kwa mara nchini Congo

Ndege moja ya umoja wa mataifa imepata ajali na kuanguka jana mjini Kinshasa na kuwaua takriban abiria thelethini na mbili.

Ndege hio ilipasuka mara mbili na kuungua moto wakati ikijaribu kutua na huku mvua kubwa ikinyesha.

Inaaminika kuwa kuna watu zaidi ya kumi wamenusurika ajali hiyo.

mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema abiria wengi walikuwa wahudumu wa tume ya umoja wa mataifa nchini humo MONUSCO wakiwemo wanajeshi wakulinda amani. Bado majina ya waliokwemo kwenye ndege hiyo hayajatolewa.

Msimamizi huduma za afya kwenye uwanja wa Ndjili mjini Kinshasa, Joseph Kiboko anasema sababu ya ajali haijajulikana lakini kunauwezekano kuwa ilisababishwa na hali mbaya ya anga.

" Kulikuwa na upepo mwingi na mvua ilikuwa inanyesha wakati ndege ilipojaribu kutua punde tuu ajali ikatokea." Bw Kiboko ameiambia BBC idhaa ya Kishwahili.

Ndege hiyo ilikuwa imeanza safari yake mjini Kisangani, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.