Huwezi kusikiliza tena

Mjadala wa katiba wafukuta Tanzania

Kikao cha bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimeanza mjini Dodoma ambapo muswada wa sheria ya mwaka 2011 kwa ajili ya kutunga sheria itakayoweka utaratibu wa kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba umewasilishwa katika kikao cha kwanza cha kikao hicho.

Huku wanasiasa na taasisi za kijamii Tanzania bara zikiwa zimeanza kulalamika juu ya mswada huo, sauti pia zimeanza kusikika Zanzibar sio tu kuupinga mswada huo lakini pia kutaka Zanzibar iwe na sauti zaidi kwenye mjadala huo.

Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa alisema Zanzibar lazima iwe na sauti yake kwenye maandalizi na hata kura ya maoni ijayo. Bwana Jussa hata hivyo amesikitika kuwa hoja yake binafasi aliyopeleka kwenye Baraza la wawakilishi imetenguliwa ambapo alitaka kusaidia Zanzibar iwe na mkono imara.

Mwandishi wetu wa Zanzibar Ali Saleh alimuuliza kwa nini hoja yake ilikataliwa na Spika wa Baraza hilo?