Miili zaidi yapatikana Ivory Coast

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mgonjwa akisubiri matibabu Abidjan

Umoja wa Mataifa umesema, zaidi ya miili 100 ilipatikana nchini Ivory Coast, huku ghasia zikiwa zinaendelea baina ya wapinzani wenye nyadhifa za Urais.

Umoja huo umesema miili hiyo ilipatikana magharibi mwa nchi hiyo, kwa kinachodhaniwa kuwa mauaji ya kikabila.

Rais anayetambulika kimataifa Alassane Ouattara amekuwa akipambana na aliye madarakani Laurent Gbagbo, aliyopo kwenye handaki mjini Abidjan.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya umesema huenda ukapunguza makali kwa upande wa vikwazo baada ya ombi lililotolewa na Bw Ouattara.

Umoja huo ulimtambua Bw Ouattara kama mshindi wa uchaguzi wa mwezi Novemba kuwa ndiye Rais lakini Bw Gbagbo amekataa kukabdhi madaraka.

Majeshi ya Bw Ouattara yamesogea toka kaskazini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita lakini eneo kubwa la mji mkuu wa Abidjan limeshikiliwa na wafuasi wa Gbagbo na siku kadhaa za mapigano imeisababishai nchi hiyo kuingia kwenye mgogor.