Mauaji Uholanzi

Mtu aliyekuwa na bunduki alifyatua risasi kati ya umati wa watu kwenye eneo la maduka nchini Uholanzi, na kuuwa watu wasiopungua 6, akiwamo yeye mwenyewe.

Haki miliki ya picha AP

Meya wa kitongoje cha Alphen aan den Rijn, karibu na Amsterdam, Bas Eenhoorn, alisema wateja wane walijeruhiwa vibaya, na wengine saba waliumia kidogo, katika kile alichoeleza kuwa machinjo.

Meya huyo alisema mshambuliaji alitumia bunduki ya rashasha na kisha akajipiga risasi mwenyewe.

Wakuu wanasema inaelekea kuwa mtu huyo hakuwa na mshirika.

Haijulikani sababu ya kufanya hayo.