Mahakama yanataka Musharraf akamatwe

Mahakama ya Pakistan, inayohusika na kupambana na ugaidi, imeiamrisha serikali kufuatilia hatua za kumkamata rais wa zamani, Pervez Musharraf.

Haki miliki ya picha AFP

Maafisa wa mashtaka wanamshutumu Bwana Musharraf kuwa hakumpa ulinzi wa kutosha kiongozi wa kisiasa, Benazir Bhutto, alipouwawa zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Mahakama hiyo maalumu ilitoa waranti mwezi wa Februari, kuidhinisha Bwana Musharraf kukamatwa.

Kiongozi huyo wa zamani wa Pakistan anaishi London, na haijulikani msimamo wa Uingereza utakuwaje.

Hakuna makubaliano ya kurejesheana wahalifu au washtakiwa.