Yanga bingwa Tanzania 2011

Yanga
Image caption Yanga ya Tanzania

Klabu ya Soka ya Yanga imetawazwa kuwa Bingwa wa ligi kuu ya soka nchini Tanzania baada ya kuifunga timu ya Toto Afrika ya nchini humo kwa jumla ya mabao 3 – 0.

Timu hiyo imekuwa bingwa baada ya kufikisha pointi 49 sawa na timu ya Simba lakini imetawazwa bigwa baada ya kuwa na uwiano wa magoli 25 na 24 dhidi ya mahasimu wao Simba.

Yanga ilikuwa ikigombea ubingwa huo baada ya kucheza mechi 22 na kufunga jumla ya mabao 32 na kufungwa mabao 8 ikifuatiwa na mahasimu wao Klabu ya Simba ambayo nayo ilikuwa ikigombea nafasi hiyo baada ya kufungana pointi.

Simba ambayo imeshika nafasi ya pili imemaliza mchezo wake wa 22 kwa kufunga mabao 39 na kufungwa mabao 17.

Kwa ubingwa huo Yanga inajihakikishia kitita cha shilingi milioni thelathini za kitanzania sawa na wastani dola 25,000 huku ikiiwakilisha Tanzania mwakani katika michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika.

Simba ambayo imeshika nafasi ya pili itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika maarufu kombe la CAF.