Mahakama yanafuta chama cha Mubarak

Mahakama ya Misri yameamrisha kuwa chama cha rais wa zamani, Hosni Mubarak, kifutwe.

Haki miliki ya picha Reuters

Mahakama ya Utawala yalisema kuwa mali ya chama cha National Democratic, pamoja na fedha na nyumba zake, zinafaa kutaifishwa na kukabidhiwa kwa serikali.

Hatua hiyo inaonekana kama inaridhia sana vugu vugu la waandamanaji, ambalo lilimlazimisha Rais Mubarak ajiuzulu.

Chama cha Bwana Mubarak, kilitawala Misri kwa zaidi ya miaka 40, baada ya kuundwa miaka ya '70, na Marehemu Anwar Sadat, aliyemtangulia Mubarak.

Bwana Mubarak na watoto wake wa kiume sasa wako kifungoni, na wanakabili mashtaka ya ulaji rushwa.