Maandamano ya Chenorbyl

Siku chache tu kabla ya kutimiza miaka 25, tangu ajali kubwa ya nuklia katika kinu cha Chernobyl, mwaka wa 1986, watu kama 2000 waliohusika na kupambana na ajali hiyo, wamefanya maandamano katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev.

Haki miliki ya picha AFP

Wanalalamika kuwa mafao na malipo ya uzeeni yamekatwa; mafao yao na maelfu wenzao, wanaolipwa kufidia kwa kuatharika na mionzi.

Serikali ya Ukraine kwa sababu ya shida za bajeti, haiwezi kuendelea kulipa fidia hizo kwa kiwango cha awali.