Israel na Hamas kusitisha mashambulio

Israel na kikundi cha Wapalestina cha Hamas, wanasema wako tayari kusitisha mashambulio ikiwa na upande wa pili utafanya vivyo.

Haki miliki ya picha AP

Msemaji wa Hamas alieleza kwamba wao hawataki mashambulio kuzidi.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Ehud Barak, alisema nchi yake iko tayari kukubali mapigano kusita endapo wapiganaji wa Gaza watamaliza mashambulio.

Ndege za Israel zimeuwa watu kama 20 katika eneo la Gaza katika majuma ya karibuni; wakati inaarifiwa kuwa wapiganaji wa Kipalestina wamerusha makombora zaidi ya mia moja eneo la kusini la Israel.

Pande zote mbili, Israel na Hamas, zimelaumiana kwa kuanza mashambulio hayo, ambayo yanasemekana kuwa makubwa zaidi tangu mashambulio ya Israeli dhidi ya Gaza, zaidi ya miaka miwili iliyopita.