Waliohudhuria maziko wameuwawa Syria

Mashirika ya kupigania haki za kibinaadamu ya Syria yanasema askari wa usalama mjini Deraa, kusini mwa nchi, wameuwa watu 26 waliokuwa kwenye maziko ya waandamanaji waliouwawa katika mapambano mengine.

Haki miliki ya picha Reuters

Mashirika hayo yanasema askari walitumia nguvu zisizostahiki, walipovunja maandamano ya amani.

Wakuu wa Syria hawakusema kitu.

Mazishi yamefanywa ya watu karibu 30 waliouwawa katika ghasia za karibuni katika mji wa Deraa na vitongoje vyake.