Mawaziri wa zamani wa Misri watashtakiwa

Mkuu wa mashtaka wa Misri amesema kuwa waziri mkuu wa zamani, Ahmed Nazif, na mawaziri wengina wawili, watafikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kutumia vibaya mali ya umma.

Haki miliki ya picha BBC World Service

Afisa mmoja amesema mashtaka hayo yanahusu manufaa ya dola milioni 15, waliyopata Bwana Nazif, Youssef Boutrous Ghali, waziri wa fedha wa zamani; na Habib al-Adli, waziri wa zamani wa mambo ya ndani ya nchi.

Mwezi uliopita, ofisi ya mashtaka yalitoa idhini kuwa Bwana Adli achukuliwe hatua za kisheria, kwa sababu ya mauaji ya waandamanaji mjini Cairo, mwezi Januari.