Maandamano yanafanywa Peshawar, Pakistan

Melfu ya watu wamekusanyika Peshawar, kaskazini-magharibi mwa Pakistan, kulalamika juu ya mashambulio yanayofanywa na ndege za Marekani zisokuwa na rubani.

Haki miliki ya picha Other

Maandamano hayo ya siku mbili, yametayarishwa na kiongozi wa upinzani, Imran Khan, ambaye anatarajiwa kuhutubia Jumapili.

Ripoti kutoka Peshawar zinaeleza kuwa watu wengi wanaendelea kuwasili kwa mabasi, magari na kwa miguu.

Malori yanayopeleka vifaa kwa wanajeshi wa NATO yamelazimika kusimama.

Mashambulio ya ndege yamezusha hasira na kuchochea chuki dhidi ya Marekani.