Sheria za dharura zitafutwa Syria

Rais Bashar al Assad wa Syria ametangaza kuwa hali ya dharura, iliyokuwako nchini kwa miongo kadha, itaondoshwa juma lijalo.

Haki miliki ya picha AP

Katika hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni, aliyotoa kwa baraza jipya la mawaziri, Rais Assad alisema hatua hiyo, ambalo lilikuwa moja kati ya madai makubwa katika maandamano dhidi ya serikali, itazidisha umoja nchini.

Sheria mpya kuhusu usalama zitaanzishwa badala hali ya dharura.

Piya alisema kutaundwa tume itayotazama kuanzishwa kwa vyama vingi vya kisiasa nchini Syria, na aliwasihi mawaziri kusikiliza madai ya haki ya watu.

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika tena katika barabara za miji ya Deraa na Banias kueleza madai yao.