Wanigeria wanamchagua rais

Uchaguzi wa rais wa Nigeria unafanywa leo, uchaguzi mkubwa kabisa kufanyika Afrika, kutokana na idadi ya watu wataoshiriki.

Watu milioni 73 wamejiandikisha kupiga kura.

Haki miliki ya picha AP

Wapigaji kura wameanza kukaguliwa, kabla ya kuanza kupiga kura mchana. Mpinzani mkubwa wa rais wa sasa, Goodluck Jonathan, anatarajiwa kuwa kiongozi wa zamani wa kijeshi, Muhammadu Buhari.

Siku ya Ijumaa na Jumaosi, kumetokea miripuko miwili ya mabomu katika mji wa Maiduguri, kaskazini-mashariki mwa nchi.

Kulitokea miripuko ya mabomu kwenye mji huo, hata wakati wa uchaguzi wa wabunge, juma lilopita.

Hata hivo uchaguzi wa wabunge ulisifiwa na wasimamizi wa uchaguzi, na matumaini ni makubwa kwa uchaguzi wa leo piya, ingawa wasi wasi ungalipo kwamba fujo zinaweza kuzuka.

Shirika la kupigania haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, linasema karibu watu 100 wameuwawa katika kampeni za uchaguzi.